You are currently viewing WILLY PAUL APEWA SOMO NA MASHABIKI KISA KIKI

WILLY PAUL APEWA SOMO NA MASHABIKI KISA KIKI

Baadhi ya wadau wa muziki nchini wamewatolea uvivu msanii Willy Paul baada ya mkali huyo kuonekana kutengeneza matukio kwa ajili ya kutangaza kazi yake mpya ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.

Kupitia mitandao yao ya kijamii wamwataka Willy Paul waache suala la kuendekeza kiki kwenye muziki wao na badala yake atoe muziki mzuri ambao utajiuza wenyewe.

Aidha wametoa changamoto kwa Bosi huyo Saldido kuwa mbunifu kwenye ishu ya kutengeneza matukio yatakayomfanya azungumziwe mtandaoni kwani kiki anazozitengeneza hazijafikia viwango vya kuteka hisia za watu.

Kauli hiyo ya wadau hao wa muziki imekuja mara baada ya Willy Paul kurekodi video akidai kuwa kuna baadhi ya wasanii wanahujumu juhudi zake za kuupeleka muziki wake kimataifa kwa kumfanyia vitendo vya kishirikina.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke