You are currently viewing WILLY PAUL APOTEZA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 96 BAADA YA TUHUMA ZA UBAKAJI KUIBULIWA DHIDI YAKE

WILLY PAUL APOTEZA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 96 BAADA YA TUHUMA ZA UBAKAJI KUIBULIWA DHIDI YAKE

Staa wa muziki nchini Willy Paul amedai kwamba amepoteza takriban shillingi millioni 96 tangu diana marua amtuhumu kuwa alijaribu kumbaka.

Kupitia waraka aliyochapisha kwenye ukurasa wake Instagram Willy Paul amesema amepoteza matangazo ya takriban shillingi millioni 10 kutoka kwa kampuni moja ya mawasilioni, shillingi milioni 4 kutoka kwa kampuni ya magodoro na dili la kurekodi na kusambaza muziki la takriban shillingi millioni 82 .

Ameenda mbali zaidi na kutoa onyo kwa Diana Marua na baadhi ya watu wanaolenga kumshusha kimuziki kwa kusema kwamba mrembo huyo amewalipa baadhi ya wanawake watoe ushahidi wa uongo dhidi yake. 

Hitmaker huyo wa “My Woman” katika taarifa yake amesema hatorusu baadhi ya watu wamharibie chapa yake ya muziki huku akidokeza kwamba atafungua kesi dhidi ya Diana Marua ambaye kwa mujibu wake analenga kumharibia kazi ya muziki kwa tuhuma za uongo.

Hata hivyo baadhi ya wadau wameonekana kutofautiana na Wiily Paul ambapo baadhi wamedai msanii huyo ameghushi kiasi hicho cha fedha huku wengine wakidai kwamba yeye ndiye alianzisha sakata hilo hivyo apambane nalo hadi mwisho.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke