You are currently viewing WILLY PAUL ASHANGAZWA NA VIEWS ZAKE KUSHUKA YOUTUBE

WILLY PAUL ASHANGAZWA NA VIEWS ZAKE KUSHUKA YOUTUBE

Staa wa muziki nchini Willy Paul amefunguka na kuzungumzia ishu ya kupungua kwa idadi ya viewers wanaotazama video za nyimbo zake kwenye mtandao wa Youtube.

Kupitia  Youtube live Willy Paul amedai kuwa kuna mchezo mchafu ambao unaendelea kwenye channel yake ya YouTube  ambapo amelalamika kuwa views za video za nyimbo zake zinapanda na kushuka.

Hitmaker huyo wa “My Woman” amesema kuna msanii ameamua kusambaratisha harakati zake za kuupeleka muziki wake kimataifa kwa kununua baadhi ya watu ambao amedai wameweka kizuizi kwenye channeli yake ya Youtube ili watazamaji wa nyimbo zake wazipande.

Hata hivyo ametoa onyo kwa msanii huyo ambaye hajamtaja jina kuacha tabia hiyo la sivyo atamwaanika ikizingatiwa kuwa ana idhibati inaonyesha kuwa amekuwa akinunua views youtube.

Kauli hiyo ya Willy Paul imetafsiriwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii  kuwa ina mlenga moja kwa moja msanii mwenzake Bahati na mkewe Diana Marua ambao katika siku za hivi karibu hajakuwa na maelewano mazuri naye.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke