You are currently viewing WILLY PAUL ATAMANI KUINGIA KWENYE NDOA

WILLY PAUL ATAMANI KUINGIA KWENYE NDOA

Staa wa muziki nchini Willy Paul ameweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye ndoa.

Kupitia instagram yake Willy Paul ameposti picha akiwa amevalia vizuri na kusindikiza na caption inayoelezea hisia yake ya kutamani kuoa hivi karibuni na mwanamke wa ndoto yake.

“Kijana ya salome anapanga kuoa.. shida yake ni, anependa kuvaa vizuri sana… atawezana na ndoa kweli??”, Ameandika Instagram.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Toto hajaweka bayana kama kweli analifanyia kazi jambo hilo ila mashabiki wamempongeza kwa hatua hiyo ya kutaka kuingia kwenye ndoa huku wengi wakimshinikiza afanye hivyo kwani ametosha kabisa kuwa mume wa mtu.

Hata hivyo wajuzi wa mambo wanahoji kuwa huenda msanii huyo anatumia suala hilo kutangaza wimbo wake mpya ambao utatoka hivi karibuni.

Ngoma ya mwisho Willy paul kuachia ilikuwa “Chocolate” ambayo kwa sasa inafanya vizuri youtube kwani ndani ya miezi 2 imeweza kutazamwa mara millioni 1.2.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke