Nyota wa muziki nchini Willy Paul ameingia kwenye headlines kwa mara nyingine, mkali huyo kwa sasa amekuwa ni mtu wa kutupa Breaking News kila uchao hii ni baada ya kusema kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza Kenya kushika namba moja kwenye mtandao maarufu duniani wa The Shaderoom kupitia single yake “I DO.”
Kupitia instastory yake Willy Paul ameeleza kuwa wimbo huo pia ulishika nafasi ya pili kwenye mtandao wa Apple TV USA lakini hakuna blogu yeyote nchini iliandika kuhusu mafanikio yake hayo kwa sababu kipindi hicho hakuwa msanii wao pendwa.
Hata hivyo, ameenda mbali zaidi na kutamba kuwa mwakani anaenda kuandika historia yake kipekee kwenye muziki wake huku akiwasihi mashabiki wamuunge mkono katika harakati za kuupeleka muziki wa Kenya kimataifa la sivyo atajipambania mwenyewe na mtu asije akafurahia juhudi zake.
Kauli ya Willy Paul inakuja siku chache mara baada ya kujinasibu kuwa yeye ndio msanii pekee kutoka Afrika Mashariki ambaye ana ngoma ambayo imepenya Kimataifa huku akiutaja wimbo wake wa “I DO” kama wimbo ambao unapigwa duniani kote.