Ikiwa tunaelekea mwishoni mwa mwaka 2022, Msanii Willy Paul amefunguka kubadili aina maisha yake mwaka 2023.
Kupitia instastory yake msanii huyo ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba amechukua hatua hiyo kuwaepuka marafiki wanafiki waliokuwa wanamtafuta kipindi cha matatizo.
Bosi huyo wa Saldido amesema mwaka huu umempa funzo kuwa mtu maarufu huwa na marafiki pale tu anapokuwa juu lakini akipata matatizo hutengwa na hata watu wake wa karibu.
Hata hivyo amesema watu pekee ambao atawapa kipaumbele maishani mwake kama marafiki zake wa dhati mwaka 2023 ni mama yake mzazi pamoja na watoto wake.