You are currently viewing WILLY PAUL ATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9 NCHINI KENYA

WILLY PAUL ATANGAZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9 NCHINI KENYA

Msanii nyota nchini Willy Paul amezua mjadala mzito kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumtawaza kinara odm Raila Odinga kuwa rais wa tano wa Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Kupitia ukurasa wa Instagram Willy Paul ameweka wazi msimamo wake wa kisiasa bila uwoga kwa kuchapisha bango la kiongozi huyo wa Chama cha ODM, jambo linalotafsiriwa moja kwa moja kuwa hitmaker huyo wa Toto amejiunga rasmi na muungano wa Azimio la Umoja ambao unampigia debe Raila Odinga kutua uongozi wa nchi ya Kenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu     .

Kauli hiyo ya Willy Paul imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kukerwa na hatua ya msanii huyo kujihusisha na masuala ya kisiasa huku wengine wakimtaka aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutoa muziki.

Utakumbuka Willy Paul ambaye anamezea kiti cha ubunge eneo la Mathare Kaskazini juzi kati aliweka wazi kuwa yupo tayari kumenyana na wagombea wenzake kutoka eneo la mathare kaskazini kwenye uchaguzi wa mchujo wa chama cha ODM Aprili 17 mwaka huu wa 2022.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke