Staa wa muziki nchini Willy Paul amewapa mashabiki wake orodha nzima ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya “The African Experience”.
“The African Experience” ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na wengine.
Hitmaker huyo wa “Lenga” anatarajiwa kuiachia album hiyo wakati wowote kuanzia sasa kwani ni saa chache tu zimesalia..
Hata hivyo Willy Paul tayari ameachia video ya wimbo mmoja kutoka kwenye album hiyo ambao ni “Ogopa Wasanii”, wimbo namba 11.