You are currently viewing WILLY PAUL AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI KENYA

WILLY PAUL AWACHANA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI KENYA

Staa wa muziki nchini Willy Paul amewatolea uvivu mapromota wa muziki nchini kwa madai ya kuwadhulumu wasanii wa kenya wanapowaalika wasanii wa nje kufanya matamasha ya muziki nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba kuna kipindi karibu avunjwe mgongo na mabaunsa kwenye harakati za kumpokea msanii wa Tanzania aliyekuwa amealikwa kwenye tamasha moja la muziki jijini Nairobi.

Hitmaker huyo wa “Heartbreak” ameenda mbali zaidi na kuwataka mapromota kuwaheshimu wasanii wakenya  na mashabiki kwani ni binadamu kama wasanii wa mataifa mengine.

Kauli ya Willy Paul imekuja mara baaada member wa zamani wa Camp Mulla, Miss Karun kuweka wazi namna waandaji wa show ya msanii wa Nigeria Omah Lay walivyomdhulumu na kumzuia kuingia kwenye eneo ambalo wasanii wenzake walipokuwa wameketi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke