Staa wa muziki nchini Willy Paul amewajibu wanaomsema vibaya mtandaoni kuwa ana kiburi tangu aanze kupata mafanikio kwenye muziki wake.
Kupitia Instastory yake amesikitishwa na madai hayo kwa kusema kuwa ana haki ya kuwa na majivuno kwa sababu anajikimu kimaisha bila usaidizi wa mtu yeyote huku akitamba kuwa yeye ni msanii mwenye kipaji zaidi nchini Kenya.
“Ati nikona kiburi?? Waah sio poa, but si kila mmoja na maisha yake? Si hakuna mtu ananilisha? Alafu si nikona chapa na life fiti alafu mimi ni sexy luo?? Plu I’m the most talented musician hapa Kenya.” Ameandika.
Ujumbe wake huo umeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wamemtaka aache masuala ya kulalamika kila mara anapokosolewa mtandaoni kwani anajidhalalisha kwa mashabiki zake kwa kuonyesha mapungufu yake.
Ukumbukwe tangu Willy Paul ajiondoe kwenye muziki wa injili na kugeukia muziki wa kidunia amekuwa akipokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya mashabiki kutokana na matukio ambayo msanii huyo amekuwa akijihusisha kwenye muziki wake.