You are currently viewing Willy Paul awapa somo wasanii wa Kenya kwa kuiga muziki wake

Willy Paul awapa somo wasanii wa Kenya kwa kuiga muziki wake

Bosi wa Saldido International, Msanii Willy Paul ameibuka na kutema nyongo kwa wasanii wa Kenya kwa kile anachokitaja kuwa wamekosa ubunifu kwenye muziki wao.

Kupitia instastory yake Hitmaker huyo wa “Tamu Walahi” ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa wasanii wengi katika siku za karibuni wamekuwa wakimuiga kwenye suala la utoaji wa nyimbo, kitendo ambacho amehoji kuwa imemfanya kusitisha mchakato mzima wa kuachia ngoma zake kwa ajili ya kuwapisha wasanii hao kuachia kazi zao.

Hata hivyo walimwengu wamehoji kuwa huenda ujumbe huo unamlenga Mr. Seed ambaye juzi kati aliachia wimbo wake “Dawa ya Baridi Remix” akiwa amemshirikisha msanii wa Nigeria, Guchi ambaye kipindi cha nyuma Willy Paul alidokeza kuwa ana wimbo wa pamoja naye.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke