Nyota wa muziki nchini Willy Paul anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yake ya “The African Experience” ambayo tayari ina takriban mwezi mmoja tangu itoke rasmi.
Album ya “The African Experience” ambayo ndio albamu ya pili kwa Willy Paul tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha zaidi ya Streams millioni moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.
Ikumbukwe album ya “The African Experience” kutoka kwa mtu mzima Willy Paul iliachiwa rasmi Oktoba 21 mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 17 ya moto huku ikiwa na kolabo 9 pekee.