Nyota wa muziki nchini Willy Paul ameamua kuwekeza kwenye biashara ya uchukuzi maarufu matatu kama njia ya kutanua kitega uchumi chake.
Akizungumza na wandishi wa habari, Willy Paul amesema kuwekeza kwenye sekta ya matatu ni moja kati ya ndoto ambazo amekuwa akitamani kufanikisha katika maisha.
Hitmaker huyo wa toto ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye masuala ya ujasirimali, amesema licha ya watu kumponda mtandaoni kuwa anapenda maisha ya starehe na anasa, amefarijika sana kutengeneza nafasi ya ajira kwa vijana wenzake kupitia uwekezaji wake huo.
Licha ya mashabiki kumpongeza kwa mafanikio hayo, kuna baadhi ya walimwengu walimrushia vijembe mtandaoni wakidai kuwa Willy Paul ameishusha chapa yake (brand) kwa hatua ya kununua gari ambalo limetumika.
“How does such a big brand in Kenya buys used car for business?” Shabiki ameandika kwenye posti ya Willy Paul Instagram.
Tayari Willy Paul amenunua magari manne aina ya matatu na amezindua gari moja liitwalo Saldido Van ambayo itajihusisha na masuala ya kusafirisha watu kwenye shughuli zao za kibinafsi.