You are currently viewing WILLY PAUL: MIMI NA DIAMOND NDIO WASANII PEKEE TUNAOWAKILISHA AFRIKA MASHARIKI KIMATAIFA

WILLY PAUL: MIMI NA DIAMOND NDIO WASANII PEKEE TUNAOWAKILISHA AFRIKA MASHARIKI KIMATAIFA

Staa wa muziki nchini Willy ameingia kwenye headlines mitandaoni mara baada ya kujigamba kuwa yeye na Diamond Platinumz ndio wasanii pekee wanaowakilisha Afrika mashariki kimataifa kupitia muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mkali huyo wa ngoma ya Toto ameeleza kwamba yeye na Diamond Platnumz ndio wanamuziki ambao wana uwezo wa kupeleka mbali zaidi muziki wa Afrika Mashariki huku akiwataja Davido na Wizkid kuwa tayari wameshafanya hivyo kwa Nigeria na ukanda wao wa Afrika Magharibi.

Hata hivyo amehapa kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba anaupigania muziki wa Afrika mashariki ufike mbali zaidi huku akiwatolea uvivu wasanii wenzake waache kulaza damu na badala yake watie bidii kwenye kazi zao za ili muziki wa ukandu huu uweze kufika mbali zaidi.

Kauli hiyo ya Willy Paul imeibua mjadala mzito miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kupuzilia mbali kauli hiyo kwa kusema kwamba msanii huyo anatafuta kiki kwa ajili ya kuachia wimbo wake mpya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke