You are currently viewing WIMBO MPYA WA MEJJA WAFUTWA YOUTUBE

WIMBO MPYA WA MEJJA WAFUTWA YOUTUBE

Staa wa muziki nchini Mejja amepata pigo nyingine mara baada ya video ya wimbo wake mpya uitwao Maisha tiki kufutwa kwenye mtandao wa youtube.

Video ya wimbo huo umeondolewa kwenye mtandao huo siku chache baada ya mejja kuweka wazi kwamba kuna mtu amewasilisha lalama ya hakimili dhidi ya wimbo wake huo kwa uongozi wa youtube.

Mejja aliachia wimbo huo Ijumaa wiki iliyopita kusherehekea hatua ya rais uhuru kenyatta kuondoa kafyu na wakati ulifutwa kwenye mtandao wa youtube ulikuwa umefikisha zaidi ya views laki moja.

Hata hivyo mashabiki zake kwenye mitandao ya kijamii wameelezea kusikitishwa na kasumba ya watu ambao wamekuwa na mazoea ya kuripoti na kudai umiliki wa nyimbo za Mejja kwenye mtandao wa Youtube huku wakitaka bodi zinazosimamia kazi za wasanii kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaoendeleza kadhia hiyo.

Huu sio wimbo wa kwanza kwa mejja kushushwa kwenye mtandao wa YouTube kwani mwezi Juni mwaka huu, nyimbo zake mbili, ‘Tabia za Wakenya’ na ‘Naitwa Mejja’ aliomshirikisha Nasha Travis pia ziliondolewa kwenye mtandao wa YouTube kwa madai ya hakimiliki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke