You are currently viewing WIMBO WA MARIOO “MI AMOR” WAFIKISHA STREAMS MILIONI 10 BOOMPLAY

WIMBO WA MARIOO “MI AMOR” WAFIKISHA STREAMS MILIONI 10 BOOMPLAY

Disemba 24 mwaka wa 2021 Staa wa muziki wa Bongofleva Marioo alitubariki na singo inayokwenda kwa jina la “Mi Amor” akiwa amemshirikisha msanii wa kike nchini Jovial.

Habari njema kwa mashabiki wa Marioo ni kwamba Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya streams millioni 10 kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay.

Sanjari na hilo wimbo wa “Mi Amor” pia unazidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa youtube kwani mpaka sasa video yake imeweza kutazamwa zaida ya mara millioni 3.3 tangu ipakiwe kwenye mtandao huo Februari 25, 2022.

“Mi Amor” unakuwa wimbo wa kwanza kutoka kwa Marioo kuwa na idadi hiyo kubwa ya STREAMS, ikizipita nyimbo kama “For You” wenye streams Milioni 4.9 ulitoka mwaka jana, “Beer Tamu” wenye streams Milioni 3.8 na watatu katika top 3 ya kazi za Marioo ilizofikisha streams zaidi ya Milioni ni “Mama Amina” wenyewe una streams Milioni 1.6

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke