Video ya Wimbo wa Vera Sidika ‘Popstar’ unatajwa kuwa video ya muziki isiyopendwa zaidi nchini Kenya kwenye mtandao wa YouTube.
Kulingana na program ya Dislike Viewer plugin, Video ya wimbo huo ,imepata zaidi ya dislikes 39,000, ikiipiku video ya Willy Paul ‘Lamba Nyonyo’ iliyotoka miaka 3 iliyopita ambayo ina zaidi ya dislikes 38,000,
Vera Sidika aliachia video wimbo wa ‘Popstar’ Oktoba 7 2022 baada ya kudai kufanya upasuaji wa kupunguza makalio yake akiwa na lwngo ya kutangaza wimbo wake mpya.