You are currently viewing WINNIE NWAGI AAPA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA NIGERIA

WINNIE NWAGI AAPA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA NIGERIA

Staa wa muziki kutoka Uganda Winnie Nwagi amefunguka kuhusu kufanya kazi na wasanii wa Nigeria.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Nwagi amesema hatokuja kufanya muziki na wasanii wa nigeria kwa kuwa wanapenda sana kuwatumia wasanii wa mataifa mengine kujitafutia makuu.

Msanii huyo wa Swangz Avenue amesema wanigeria wamekuwa na mazoea ya kuwatumia wasanii wengi vibaya kusukuma brand au chapa yao ya muziki  katika soko la uganda lakini nchini kwao hawatangazi kazi za waganda.

Utakumbuka Winnie Nwagi amewahi kufanya kazi na mwanamuziki kutoka Nigeria Slim Prince kupitia ngoma yao inayokwenda kwa jina la Fire Dance.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke