Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu tetesi za lebo hiyo kumpendelea msanii mwenzake Azawi huku wakimtenga.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Winnie Nwagi amewatolea hofu mashabiki zake kwa kusema kuwa yupo mbioni kuja na onesho lake ambalo ana imani kuwa itapata mapokezi makubwa.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malaika” amesema hana la kusema kuhusu tamasha la Azawi linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa sababu kila mtu katika maisha ana bahati na muda wake.
Kauli ya Winnie nwagi imekuja mara baada ya mashabiki kuisuta vikali lebo ya swangz avenue kwa hatua ya kumuandalia onesho la muziki msanii Azawihuku wakimuacha pembeni winnie nwagi ambaye amekuwa chini ya lebo hiyo kwa muda mrefu.