You are currently viewing WINNIE NWAGI AFUNGUKA TUHUMA ZA KUKATAA KULIPA KIINGILIO KWENYE MOJA YA NIGHT CLUB

WINNIE NWAGI AFUNGUKA TUHUMA ZA KUKATAA KULIPA KIINGILIO KWENYE MOJA YA NIGHT CLUB

Mwanamuziki kutoka Uganda Winnie Nwagi amejibu tuhuma za walinzi kumzuia kuingia kwenye moja ya klabu ya usiku huko Kololo nchini Uganda baada ya kususia kulipa kiingilio.

Kwenye video aliyoposti Snapchat Nwagi mrembo huyo amekiri kuzozana na walinzi wa club hiyo kwa kusema kuwa alishangazwa na hatua yao kumtaka alipe kiingilio wakati nyimbo zake zimekuwa zikipigwa kwenye eneo hilo la burudani.

Hitmaker huyo wa “Malaika” amesisitiza kuwa wasanii wanapaswa kupewa heshimu kwa kazi zao za muziki badala ya kukandamizwa.

Kauli ya Winnie Nwagi imekuja mara baada ya chanzo kimoja kukiambia jarida moja la habari nchini Uganda kuwa msanii huyo pamoja na marafiki zake watano walizuiliwa kuingia kwenye club moja ya usiku kwa madai ya kukataa kulipa kiingilio.

Chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kumtaka Winnie Nwagi aheshimu biashara za watu licha ya kuwa mtu maarufu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke