You are currently viewing WINNIE NWAGI AJITAPA KUFANYA TAMASHA LAKE BILA MATANGAZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI

WINNIE NWAGI AJITAPA KUFANYA TAMASHA LAKE BILA MATANGAZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi juzi kati alitangaza kufanya tamasha lake la muziki Septemba 9 mwaka huu huko Cricket Oval Lugogo viungani mwa jiji la Kampala.

Hii ni baada ya Swangz Avenue kuitikia mwito wa mashabiki ambao walikuwa wanaipa shinikizo lebo hiyo kuandaa tamasha la msanii huyo kutokana na wao kuonekana kuwapendelea wasanii Vinka pamoja na Azawi.

Licha ya kwamba Winnie Nwagi hanaitaji vyombo vya habari kutangaza tamasha lake lijalo liwafikie wengi mrembo huyo amejitokeza na kujinadi kuwa haitaji usaidizi wa mtu yeyote ndio aweze kujaza ukumbi wa Cricket oval kwani ana uwezo wa kufanya hivyo mwenyewe kutokana na alama ambayo ameiacha kwenye tasnia ya muziki kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

“I don’t need you to advertise for me. I can pull it off without publicity,” Winnie Nwagi amejibu shabiki kwenye mtandao wa twitter ambaye alichapisha ujumbe kuhusu onesho lake la muziki.

Kwa miaka kadhaa sasa winnie nwagi amegonga vichwa vya habari kutokana matukio yake ya kushangaza ikiwemo kumshushia kichapo mfanyikazi wake wa nyumbani, kuvalia mavazi yanaonyesha uchi wake, na kuwatusi wakosoaji wake kwenye mitandao ya kijamii.

Tunaamini miendo yake isiyoridhisha haitafanya mashabiki kutohudhuria tamasha lake la muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke