Mwanamuziki Winnie Nwagi ameshinndwa kuficha furaha yake mara baada ya kuwapata wafadhili wa tamasha lake la muziki linalotarajiwa kufanyika Septemba 9 katika ukumbi wa Oval Criket huko Lugogo viungani mwa jiji la Kampala.
Kwenye mkao na waandishi wa habari, Winnie Nwagi amesema aliingiwa na hofu baada ya wafadhili kushindwa kujitokeza alipotangaza ujio wa tamasha lake hilo.
“Niliogopa sana. Unajua gharama zinaweza kuwa kubwa lakini nilijua nitapata wadhamini wazuri na namshukuru Mungu nilipata.”
Nwagi hadi sasa ameukaribisha udhamini wa chapa ya bia, iitwayo Club beer, na vituo vya redio nchini Uganda licha ya kushindwa kupata wafadhili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja alipotoa tangazo kuhusu tamasha lake la muziki.