You are currently viewing WINNIE NWAGI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE

WINNIE NWAGI AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI KWENYE MOJA YA PERFORMANCE

Winnie Nwagi ni moja kati ya wasanii ambao watu wengi nchini Uganda wanamtaja kama malkia wa kashfa nchini humo kutokana vituko vyake.

Wikiendi hii iliyopita kwenye moja ya performance yake alimsaba makofi shabiki yake mmoja ambaye alijaribu kumchukua video akiwa jukwaani bila ridhaa yake.

Kwenye moja ya video inayosambaa mitandaoni Winnie Nwagi anaoneka akimshushia kichapo cha mbwa shabiki yake huyo kwa kumsaba makofi matatu ya moto.

Kutokana na hilo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahishwa na kitendo hicho ambapo wamemtaka winnie nwagi akome kuwashambulia mashabiki ambao ukoshwa na mtindo wa mavazi yake ambayo mara nyingi uonesha maungo yake ya mwili kwa umma.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wametishia kususia matamasha yake ya muziki iwapo ataendelea na kasumba hiyo ya kuwavamia mashabiki wanaomuunga mkono kwenye muziki wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke