Msanii kutoka Uganda Winnie Nwagi ameingia kwenye headlines mara ya kudaiwa kukwepa kulipa deni la shillingi elfu tisa analodaiwa na night club moja nchini humo.
Kulingana na vyanzo vya karibu na night club hiyo, Nwagi amekuwa akila chakula pamoja na kuagiza vinywaji kwa kipindi cha miezi mitatu bila malipo yeyote.
Chanzo hicho kimeenda mbali na kudai baada ya uongozi night club hiyo kumtaka alipie gharama ya huduma aliyopewa, alihamua kuingia na jeuri kiasi cha kumtishia maisha mmiliki wa eneo hilo la burudani.
Hata hivyo ni jambo ambalo lilipelekea uongozi wa night club hiyo kukata mshahara wa mfanyikazi aliyemhudumia Winnie Nwagi kwa ajili ya kukamilisha deni hilo.