You are currently viewing WINNIE NWAGI MBIONI KUACHA MUZIKI

WINNIE NWAGI MBIONI KUACHA MUZIKI

Inaonekana msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi hana furaha kwa sasa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Kulingana na posts zake kwenye mitandao ya kijamii hitmaker huyo wa “Musawo” inaonekana anapitia kipindi kigumu kwenye maisha yake ambayo hajawahi kutana nayo tangu aanze safari yake ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa twitter mrembo huyo amesema kwamba kama angekuwa na kitu kingine cha kufanya kwenye maisha, angeacha muziki kabisa.

Winnie nwagi amesema amechoshwa na kile kinachoendelea kwenye maisha yake kwa sasa a ameomba dua kwa mwenyezi mungu aingilia maisha yake kabla hajachukua maamuzi magumu.

Kuthibitisha kwamba Winnie Nwagi hana furaha kabisa alienda mbali zaidi na kuwablock mashabiki wake wote kwenye mtandao wa instagram wasiweze ku comment kwenye post yake.

Hata hivyo mrembo huyo hajaweka wazi kinachomsumbua kwa sasa kwenye maisha yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke