Wizkid ameandika rekodi mpya kwenye muziki wa Afrika, album yake “Made In Lagos” imetajwa kuwania kipengele cha Album Bora ya Mwaka kwenye Tuzo za Soul Train Awards za nchini Marekan. Hivyo imekuwa album ya kwanza ya Kiafrika kwenye historia kutajwa kwenye kipengele hicho.
Rekodi ya pili Wizkid imeiweka kupitia wimbo wake wa Essence ambao umekuwa wimbo wa kwanza wa Kiafrika kuingia kuwania vipengele vya Song of The Year, Video of The Year, Best Collaboration lakini pia kwenye kipengele cha The Ashford and Simpson’s Songwriter’s Award.
Wizkid atachuana na wakali kama Doja Cat, H.E.R, Jazmine Sullivan, Bruno Mars, Chris Brown na wakali wengine kwenye vipengele hivyo.
Soul Train Awards ni Tuzo za muziki ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani kuwatunuku African-American kwenye nyanja za muziki na burudani. Tuzo za mwaka huu zitafanyika November 20.