You are currently viewing WIZKID ATAJWA KAMA MSANII KINARA ROLLING LOUD

WIZKID ATAJWA KAMA MSANII KINARA ROLLING LOUD

Mwanamuziki kutoka Nigeria Wizkid ametajwa kwenye orodha ya wasanii watatu vinara (headliners) ambao watatumbuiza kwenye tamasha la Rolling Loud ambalo litafanyika September 9 hadi 11 mwaka huu mjini Toronto, Canada.

Mbali na Wizkid kuna wasanii kama Future na Dave ambao ndio wanakamilisha idadi ya headliners watatu wa tamasha hilo lenye mamia ya wasanii wakali kutoka nchini Marekani ambao watapanda Jukwaani.

Kubwa hapa ni kiasi cha pesa ambacho Wizkid amelipwa kutumbuiza kama msanii kinara, kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram amesema amelipwa million 115 za Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke