Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid anaendelea kuchana mbuga Kimataifa mara baada ya kutangazwa kuwania tuzo za Billboard Music Awards kwenye kipengele cha Top R&B Song kupitia REMIX ya wimbo wake ‘Essence’ aliyomshirikisha Justin Bieber pamoja na Tems.
Wizkid ambaye ni mshindi wa tuzo tatu za Billboard kupitia wimbo wa Drake ‘One Dance’ kolabo ambayo ilibeba tuzo hizo 3 usiku wa Mei 21, mwaka 2017.
Hii inakuwa mara yake ya 8 kuingia kwenye nominations za tuzo hizo maarufu nchini Marekani.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mei 16, huko Marekani, na mwaka huu wasanii The Weeknd, Doja Cat na Justin Bieber wakiongoza kuwa na nominations nyingi zaidi.