You are currently viewing WIZKID ATAJWA KUWANIA VIPENGELE VIWILI VYA TUZO ZA GRAMMY

WIZKID ATAJWA KUWANIA VIPENGELE VIWILI VYA TUZO ZA GRAMMY

Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid ametajwa kwenye vipengele viwili vya tuzo za Grammy mwaka wa 2022.

Wizkid atawania kipengele cha Best Global Music Perfomance kupitia wimbo wake wa ‘Essence’ aliyomshirikisha Tems na pia kipengele cha Best Global Music Album kupitia album yake, Made In Lagos.

Hii ni mara ya kwanza kwa Wizkid kutajwa kwenye ‘mainstream category’ ukiacha kutajwa kama mshiriki kwenye Kolabo ya ngoma kama “Brown Skin Girl” na album ya Drake ‘Views’ ya mwaka wa 2016.

Wakali wengine kutoka Afrika ambao wametajwa kwenye tuzo hizo ni Burna Boy, Femi Kuti, Made Kuti na Angelique Kidjo ambao pia wanawania vipengele hivyo hivyo.

Burna Boy ametajwa kwenye ngoma aliyoshirikishwa na Angelique Kidjo, Do Yourself. Black Coffee pia ametajwa kuwania kipengele cha Best Dance/Electronic Album kupitia album yake ya Sub-consciously.

Tuzo hizo za 64 zitafanyika Januari 31, mwaka wa 2022 katika ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles nchini Marekani

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke