Staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid amethibitisha rasmi kukamilisha album yake mpya aliyoipa jina “More Love, Less Ego”.
Kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa instagram wizkid amesema album hiyo itatoka hivi karibuni.
Hata hivyo Wizkid bado hajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia album hiyo mpya lakini ametoa shukrani kwa wote waliohusika katika uandaaji wake.
Album hii mpya itaifuata “Made In Lagos” ambayo ilitoka Oktoba 30, mwaka 2020.