Hitmaker wa “Essence”, Msanii Wizkid ameviteka vichwa vya habari vya mitandao yote ya burudani, hii ni kufuatia kauli yake kwamba Muziki wa Hip Hop umekufa. Kwenye mahojiano na 10 Magazine, Wizkid amekaririwa akisifia ukuaji wa muziki wa Afrobeats Kimataifa huku akiuponda Muziki wa Rap.
Mwanamuziki huyo kutoka Nigeria amesema mbali na Afrobeats, huwa hasikilizi aina nyingine ya Muziki hasa Rap kwa sababu nyimbo nyingi zinazotengenezwa zinaboa.
Hata hivyo hakuishia hapo, aliendelea na mashambulizi yake juu ya Hip Hop ambapo alihamia kwenye mtandao wa Snapchat na kuwatolea uvivu wasanii wa Rap Afrika kwa kusema, kando na Nasty C, Sarkodie na Black Sherif wengine wote ni hovyo na ni watu waliofulia kisanaa.