You are currently viewing WYRE AWATAKA WASANII KUJIUNGA NA BODI ZA MUZIKI KENYA

WYRE AWATAKA WASANII KUJIUNGA NA BODI ZA MUZIKI KENYA

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Kenya Wyre ametoa changamoto kwa wasanii wenzake kujiunga na bodi zinazojihusisha na muziki ili kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya muziki nchini humo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Wyre amesema inasikitisha kuona wasanii wa muziki nchini Kenya wanapinga utendakazi wa bodi za muziki nchini humo wakati sio wanachama wa bodi hizo jambo ambalo anadai imekuwa vigumu kwao kutekeleza baadhi ya mabadiliko wanayotaka kwenye tasnia ya muziki.

Mbali na hayo Wyre amezindua jukwaa lake la muziki liitwalo Blow Africa litakalo toa fursa kwa wasanii chipukizi kuingiza kipato kupitia kazi zao za muziki.

Wyre amesema kwa kipindi cha miezi minane amekuwa akifanya kazi jukwaa hilo kwa ushikiriano na baadhi ya wadau wa maendeleo kuhakikisha wasanii wanaboreka kiuchumi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke