Msanii na mwaandishi wa nyimbo kutoka nchini Uganda Oman Rafiki amefunguka na kudai kuwa aliumizwa na kitendo cha msanii Vivian Tendo kujiondoa kwenye lebo ya muziki ya Route Entertainment.
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Oman Rafiki amesema licha ya kuumizwa na kitendo cha mrembo huyo kumkimbia hatokataa tamaa ya kuwasajili wasanii wapya wenye vipaji kwenye lebo hiyo.
Oman Rafiki ambaye pia ni Meneja wa wasanii amesema amejifunza umuhimu wa kuwa na mkataba wa maelewano na msanii yeyote atakajiunga na lebo ya route Entertainment kwani itamsaidia sana wakati msanii husika atajiondoa ghafla kwenye lebo hiyo.
Inadaiwa kuwa Oman rafiki na vivian tendo wamefanya kazi kwa pamoja tangu mwaka wa 2018 kwa makubaliano ya urafiki wa kimapenzi.
Hata hivyo inasemekana Vivian Tendo na Oman Rafiki wana mpango wa kuelekea mahakamani kuhusiana na hakimiliki ya muziki na masuala mengine.