You are currently viewing YG AHUSISHWA NA MAUJI YA RAPA DRAKEO THE RULER

YG AHUSISHWA NA MAUJI YA RAPA DRAKEO THE RULER

Rapa kutoka nchini Marekani YG amehusishwa na mauaji ya rapa Drakeo the Ruler ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu akiwa nyuma ya jukwaa kwenye onesho lililofanyika mjini Los Angeles, Disemba 18 mwaka huu.

Polisi bado hawajamtia hatiani mtu yeyote lakini uvumi unaosambaa mitandaoni ni kwamba YG na genge lake wamehusika na mauaji hayo.

Kwenye mahojiano na Rolling Stone, mama wa marehemu Drakeo alionekana kuwa na uhakika na YG kuhusika kumuua mwanaye kwa sababu mauaji hayo yalitokea punde tu baada ya YG kuingia nyuma ya jukwaa (backstage), Mshkaji wake Drakeo aitwaye K7 pia naye amemtaja YG.

Akiwa LIVE Instagram, K7 ameonekana mwenye hasira huku akimtaja YG na genge lake kuhusika kwa asilimia mia moja.Anasema YG alikuja na watu zaidi ya 70 backstage. Aidha alienda mbali na kutoa vitisho kwamba labda YG asitumbuize mjini Los Angeles, kwani pindi akimuona popote atalipiza kisasi.

Kisa kikubwa kinatajwa kuwa ni wivu na hofu ya YG kupitwa na Drakeo the Ruler, K7 amesema Drakeo aligoma kujiunga na genge la Bloods na kuamua kuanzisha njia yake kitendo ambacho kilimchukiza sana YG.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke