You are currently viewing YKEE BENDA AFUNGUKA SABABU ZA KUTAKA KUWA MUISLAMU

YKEE BENDA AFUNGUKA SABABU ZA KUTAKA KUWA MUISLAMU

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda ameweka wazi matamanio yake ya kubadili dini kutoka ukristo kwenda Uislamu.

Akiongea na waandishi wa habari nchini uganda, ykee benda amefichua kuwa anaipenda dini ya Kiislamu kutokana na mambo mazuri yanayoambatana nayo, ikiwa ni pamoja na kuoa wanawake wanne ambayo ni tofauti na dini nyingine.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Farmer” amesisitiza kuwa anapenda jinsi wake wenza wanavyoishi pamoja katika ndoa za Kiislamu bila ya kuwa na migogoro, jambo ambalo ni nadra katika dini nyingine.

Ykee Benda ni baba wa mtoto mmoja na uhusiano wake wa kimapenzi unaripotiwa kuwa unasuasua na ndiyo sababu anafikiria kubadili dini kuwa Muislamu.

Bosi huyo wa Mpaka Records amefunguka kuhusu nia yake ya kusilimu wakati akiwapa chakula Waislamu huko Kireka nchini uganda wakati wa sherehe za Eid.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke