You are currently viewing YKEE BENDA AGEUKIA BIASHARA YA KUANDAA MATAMASHA YA MUZIKI

YKEE BENDA AGEUKIA BIASHARA YA KUANDAA MATAMASHA YA MUZIKI

Staa wa muziki kutoka Uganda Ykee Benda ametangaza kujikita zaidi katika shughuli ya kuandaa maonesho ya muziki.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Ykee Benda amesema wameamua kuwekeza pesa zao kwenye matamasha ya muziki kwani wasanii wanaposainiwa kwenye lebo za muziki wanaleta hasara badala ya faida, kitendo ambacho kimemkatisha tamaa kwenye masuala ya kulea vipaji.

Hitmaker huyo wa “My Babe” amesema lebo yake ya Mpaka Records haitomsaini msanii yeyote katika siku za hivi karibuni  hadi pale atakapoweka mambo sawa kwa upande wake.

Utakumbuka baada ya msanii Dre Cali kujiondoa kwenye lebo ya Mpaka Records bila kufuata taratibu zinazofaa aliacha lebo hiyo ikakadiria hasara ya maelfu ya pesa kitu ambacho kimemfanya bosi wa lebo hiyo kuja na mbinu mpya kujiboresha kiuchumi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke