You are currently viewing YKEE BENDA AILILIA SERIKALI YA UGANDA KUPUNGUZA USHURU KWA HUDUMA ZA MTANDAO.

YKEE BENDA AILILIA SERIKALI YA UGANDA KUPUNGUZA USHURU KWA HUDUMA ZA MTANDAO.

Wanamuziki wa Uganda hawajaweza kuwatumbuiza mashabiki zao kwa takriban miaka miwili sasa kutokana na vikwazo vya kuzuia janga la Corona ambavyo vilipelekea kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya watu na matamasha ya muziki.

Wasanii walilazimika kubuni njia za kupata pesa kupitia mitandaoni ya ku stream muziki, na mauzo ya albamu. Lakini mapato kutoka kwa majukwaa ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni sio ya kuridhisha kwani mashabiki wachache wa muziki nchini Uganda hununua muziki mtandaoni.

Sasa katika mahojiano hivi karibuni Bosi wa Mpaka Records, msanii Ykee Benda amesema mashabiki wa muziki nchini Uganda hawasapoti wasanii kwenye majukwaa ya mitandao kwa sababu ya gharama ya juu ya vifurushi vya internet, ambavyo anadai imetokana na ushuru mkubwa.

Hitmaker huyo wa “Banange” ametoa wito kwa serikali ya uganda kupunguza ushuru inayotozwa huduma ya mtandao ili wananchi waweze kuwasapoti wasanii wa muziki nchini humo.

Ikumbukwe mapema mwezi Agosti mwaka huu Ykee Benda aliachia albamu yake ya “Kirabo” ambayo aliuza nakala 35,000 kupitia tovuti yake ambapo alifanikiwa kuuza nakala 500 wiki ya kwanza baada ya album hiyo kuachiwa rasmi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke