You are currently viewing Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Bosi wa lebo ya mpaka Records, Ykee Benda amemkingia kifua rapa Gravity Omutujju kutokana na kauli yenye utata aliyotoa juzi kati dhidi ya wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ykee amesema hatua ya Omotujju kuwataka wasanii hao kustaafu muziki na kuwaapisha wasanii wajanga ilikuwa njia ya rapa huyo kutengeneza mazingira ya kuzungumzia mtandaoni.

Ykee Benda amesema kauli ya hitmaker huyo wa “Enyama” haikulenga kumvunjia heshima msanii yeyote bali alitoa matamashi hayo kwa ajili ya kuteka hisia za mashabiki kabla kuachia wimbo wake mpya.

Hata hivyo amewalaumu wasanii wakongwe kwa kuwaaminisha wasanii wajanga kuwa hawezi toboa kisanaa bila kujihusisha na matukio yenye ukakasi.

Utakumbuka baada ya Gravity Omutujju kuwataka wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone alikashifiwa na baadhi ya wasanii pamoja na mashabiki jambo ambalo lilimlazimu kuomba radhi kwa kuwavunjia heshima wasanii hao mbele ya waandishi wa habari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke