Bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records, Wycliffe Tugume maarufu kama Ykee Benda anaamini kuwa msanii Chosen Becky hapewi heshima anaostahili kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Hitmaker huyo wa Banange amesema chosen becky ni mmoja wa wanamuziki wa kike wenye vipaji nchini humo lakini watu wamekuwa wakimchukulia poa.
Kulingana na Ykee Benda watumiaji wa mitandao ya kijamii hawathamini vipaji kwani mara nyingi wamekuwa wakitoa maneno ya kumkatisha tamaa mrembo huyo.
Kauli ya ykee benda inakuja siku chache baada ya kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook akionyesha jinsi anavyomkubali hitmaker huyo wa “Bakuza”.