You are currently viewing YKEE BENDA AVUNJA UKIMYA WAKE KUHUSU SAKATA LA MUZIKI WAKE DRE. CALI

YKEE BENDA AVUNJA UKIMYA WAKE KUHUSU SAKATA LA MUZIKI WAKE DRE. CALI

Staa wa muziki nchini Uganda Ykee Benda amevunja kimya chake kuhusu ishu ya kukosana vibaya na msanii wake Dre Cali kiasi cha kurushiana makonde walipoingia kwenye ugomvi mkali wa pesa.

Katika barua aliyochapisha kwenye mtandao wa Twitter Ykee Benda amesema hana ugomvi wowote na Dre. Cali kama inavyoripotiwa mtandaoni huku akidai kuwa lebo ya muziki ya Mpaka Records bado ina ukaribu na msanii huyo na famili yake ambapo hivi karibu  watanyosha maelezo kuhusu safari ya msanii huyo nchini Canada.

Ykee Benda kupitia barua hiyo amesema kama kutakuwepo na utofauti kati yao wawili itasuluhishwa kwa njia ya amani huku akiongeza kuwa maelezo zaidi yatawekwa wazi kwa umma hivi karibuni.

Uvumi wa Ykee Benda kutokuwa na uhusiano mzuri msanii wake Dre Cali ulianza mara baada ya msanii huyo kutoonekana kwenye afisi za lebo ya muziki ya Mpaka Records kwa muda jambo ambalo lilimlazimu Ykee Benda kuvunja kimya chake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke