You are currently viewing Ykee Benda awatambulisha wasanii wa UgaBoys kwenye lebo yake ya Mpaka Records

Ykee Benda awatambulisha wasanii wa UgaBoys kwenye lebo yake ya Mpaka Records

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Ykee Benda amewatambulisha wasanii wa kundi la Ugaboys katika lebo yake ya muziki ya Mpaka Records.

Katika mkao na wanahabari Ykee amesema ameingia ubia wa kufanya kazi na wasani wa UgaBoys kwa ushirikiano na lebo ya muziki yenye makazi yake nchini Norway, Sundance kwa ajili ya kutanua wigo wa muziki wa Uganda uweze kufika mbali zaidi.

Lakini pia amesema tayari amekamilisha michakato ya kisheria ya kufanya kazina wasanii hao chini ya Mpaka Records huku akisema kuwa ana imani nao kwani wana vipaji vya kipekee kwenye muziki wao.

Kundi la Ugaboys ambalo linaundwa na wasanii Malinga Sulaiman na Musungi Muhammmad awali walikuwa wamesainiwa chini ya lebo ya muziki ya Black Market Records lakini walikuja wakaingia kwenye ugomvi na lebo hiyo walipokwenda kinyume na mkataba wao kwa kuachia wimbo uitwao “Gimmie” waliokuwa wamemshirikisha Ykee Benda.

Utakumbuka mwaka wa 2019 Ykee Benda alimsajili msanii Dre Cali kwenye lebo yake ya Mpaka Records lakini mwaka wa 2021 baada ya kupata mafanikio makubwa kwenye muziki wake msanii huyo alivunja mkataba wao na kutumikia nchini Canada ambako anaishi kwa sasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke