Rapa kutoka nchini Tanzania Young Dee ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa Nyanguva.
Young D ambaye ni CEO wa Kampuni ya The Dream City, inayojihusisha na usimamizi wa kazi zake, amesema album hiyo imebeba jumla ya mikwaju 10 ya moto huku ikiwa na kolabo 5 pekee.
Young D amewashirikisha wasanii mbali mbali kama rapa Rosa Ree, Rapcha, Mrisho Mpoto, Linex na wengine kibao.
Album ya Nyanguva ni album ya kwanza kwa mtu mzima Young Dee na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay
Ikumbukwe album ya Nyanguva ilipaswa kuachiwa rasmi mwezi Julai mwaka huu lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa Young Dee uongozi wake uliahirisha