You are currently viewing YOUNG LUNYA AFUNGUKA MAENDELEO YA ALBUM YAKE MPYA

YOUNG LUNYA AFUNGUKA MAENDELEO YA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Hip Hop Tanzania, Young Lunya amesema albamu yake imeshamilika kwa asilimia 90, na sasa vimebakia vitu vichache vya mwisho kama mixing, mastering na kupangiwa tarehe ya kutoka na Sony Music.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Sony Music Africa Juni 3, 2022, tayari Lunya yupo kwenye maandalizi ya albamu yake ya kwanza ambayo amewashirikisha Diamond Platnumz, Khaligraph Jones, Sho Madjozi na wengineo.

Lunya amesema kufanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz, Khaligraph Jones na Sho Madjozi katika albamu hiyo ni hatua nyingine ya ukuaji wa muziki wake kibiashara na kimataifa.

“Ni hatua nzuri kufanya kazi na msanii kama Diamond kwa sababu unakuwa unafanya kazi na msanii ambaye anajua biashara ya muziki, anajua nini kinafanyika, anataka hiyo kazi ije kuwa fedha, kwa hiyo ni kitu kikubwa sana,” amesema.

“Ukija Kenya, Khaligraph Jones ni msanii anayefanya sana vizuri huko, kufanya naye kazi itanisaidia sana mimi kupenya Kenya kirahisi. Sho Madjozi wa Afrika Kusini ni msanii mkubwa kule kwao, ngoma zake zimefanya vizuri duniani, kwa hiyo ni kitu kizuri kufanya nao kazi” amesema Lunya.

Hadi sasa kwa Tanzania Young Lunya ameshafanya kolabo na wasanii kama Ommy Dimpoz, Nikki wa Pili, Mabantu, Country Boy, Maua Sama, Rosa Ree, Joh Makini, Mimi Mars, Haitham Kim, Moni Centrozone, Harmonize, Profesa Jay na wengineo

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke