You are currently viewing YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUSAINIWA ROCKSTAR

YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUSAINIWA ROCKSTAR

Rapa kutoka nchini Tanzania Young Lunya amethibitisha kusaini kufanya kazi na lebo kubwa ya muziki Afrika Rock Star ambayo pia inafanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa za muziki duniani.

Akieleza hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Young Lunya amesema mchongo huo ulikuja kupitia verse ya freestyle aliyoposti kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii.

Mkali huyo ambaye pia ni msanii bora wa Hip Hop wakiume kwa mwaka 2021 kupitia tuzo za Muziki Tanzania (TMA), lebo yake hii mpya ishawahi kufanya kazi na wasanii kama AliKiba, Baraka The Prince na Lady Jay Dee.

Kauli yake imekuja wiki kadhaa zilizopita baada ya Lebo ya Rockstar Africa kutangaza rasmi kuwasaini wasanii kutoka nchini Tanzania ambao ni Abby Chams na Aslay.

Rockstar Africa ni label inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment na ilianzishwa mwaka 2015 na Mtanzania Christine ‘Seven’ Mosha ambaye ndiye muanzilishi na mmiliki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke