You are currently viewing YOUNG THUG ASEMA ATLANTA NDIO MJI NAMBA 1 KWA HIPHOP

YOUNG THUG ASEMA ATLANTA NDIO MJI NAMBA 1 KWA HIPHOP

Kwa hapa Kenya miaka kadhaa nyuma uliibuka mjadala wa ni upi mtaa ambao ni kitovu cha Hip Hop. Mtaa wa Dandora na Kariobangi South ilikuwa kwenye ushindani mkubwa.

Kwa Marekani swali hilo pia huwa linaulizwa kwa miaka sasa, rapa Young Thug ameibuka na kusema Atlanta ndio mji namba moja kwa Hip Hop. Kwenye mkutano wa Revolt, Thug amesema “Sioni mji mwingine ukiipiku Atlanta kwa sababu tunaendelea kuibua wasanii wapya. Wasanii wakubwa wanaofanya vizuri kwa sasa wanatokea Atlanta. Juhudi zao za kushirikiana ndio zinafanya mji wetu kufanikiwa na ndio maana pia wanaendelea kukimbiza kwenye muziki na mitindo.”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke