Kuelekea event yake ya Zari All White Party inayotarajiwa kufanyika wikiendi hii Kampala, Uganda, Zari The Bosslady ametoa neno.
Zari ambaye amezaa na Staa wa Bongofleva Diamond Platnumz watoto wawili, Tiffah na Nillan, amedai yeye ndiye mrembo anayeiwakilisha vizuri Uganda.
“Mimi ndiye msichana mrembo Uganda wako naye, naiwakilisha Uganda vizuri sana.” amesema Zari The Bosslady.
Utakumbuka Zari The Bosslady, Mama wa watoto watano anayeishi Afrika Kusini na familia yake, ni mwanamke mwenye nguvu ya ushawishi Afrika Mashariki upande wa urembo na mitindo, huku akiwa na followers milioni 11.1 Instagram.