Mrembo maarufu wa Uganda, Zari The Bosslady ameonyesha kuchukizwa na habari za uongo kuhusu kile kinachodaiwa yupo katika mashindano na Zuchu ili kuunasa moyo wa Diamond Platnumz.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari amesema “Halafu wajinga wote hapa wanaamini maoni hayo yaliyoambatanishwa na picha yangu? Nimekuwa nikiwaonya kuwa siku moja nitawashtaki kiwango cha nyinyi kuuza figo zenu ili mueze kunilipa. Wacheni uongo na upuzi. Shenzi type,”
Kauli yake imekuja mara baada ya ukurasa mmoja wa Instagram kuweka picha iliyoonyesha Insta story za Zari akimsihi Zuchu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz.
Kwenye picha hiyo ‘Zari’ alisema kuwa Diamond ataishi kuwa mpenzi wake na mapenzi yake na Zuchu hayatadumu.
Kwa sasa Zari The Bosslady ambaye amekuwa anaishi Afrika Kusini na familia yake, alijaliwa watoto wawili na Diamond Platnumz, Tiffah na Nillan.