You are currently viewing ZARI AVUNJA UKIMYA TAARIFA ZA KUOLEWA

ZARI AVUNJA UKIMYA TAARIFA ZA KUOLEWA

Mrembo Zari The Bosslady amewataka mashabiki wake kupuuzia taarifa zinazodai kuwa ameolewa.

Zari ambaye ni baby mama wa msanii wa BongoFleva amesema picha hizo zinazodaiwa ni za ndoa yake, zimetoka kwenye kuandaa video ya msanii chipukizi wa muziki wa Injili.

Utakumbuka mwaka wa 2020 ilisemekana kuwa Zari pia ameolewa na mwanaume aitwaye ‘King Bae’ lakini baadaye alikuja kuweka wazi hilo halikuwa kweli.

Mwanamama huyo wa watoto watano sasa ni miongoni mwa wanawake wenye nguvu ya ushawishi Afrika Mashariki, huku akiwa na followers zaidi ya milioni 9.7 kwenye mtandao wa Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke