You are currently viewing Zari Hassan akatisha mkataba na hoteli moja nchini Uganda kwa kuvujisha picha zake za faraghani

Zari Hassan akatisha mkataba na hoteli moja nchini Uganda kwa kuvujisha picha zake za faraghani

Soshalaiti’ na mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zari Hassan amekatisha mkataba wake na hoteli moja ya kifahari nchini Uganda ambapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi wake Shakib Cham.

Zari ametangaza kuvunja mkataba wake na Divine Resort & Spa baada ya mpiga picha mmoja wa hoteli hiyo kukiuka kifungu cha mkataba wao kilichosema kwamba picha na video zote zinapaswa kuidhinishwa na Zari kabla ya kuachiwa.

“Mpiga picha huyo ameweka picha za Zari kabla ya kuidhinishwa. Kuanzia sasa, Zari hatabanwa tena na mkataba huo na hata-tag Divine Resort AndS pa kwenye chapisho zake zozote za mitandao ya kijamii,” sehemu ya barua ya kusitishwa kwa Mkataba huo imeeleza.

Katika barua hiyo, Zari ambaye ni zamani wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alitoa agizo kwa mpiga picha mhusika kufuta picha zake zote alizochapisha kwenye kurasa zake na zile ambazo alituma kwa wanablogu.

Pia, aliizuia hoteli hiyo dhidi ya kutumia picha zake na mpenzi wake kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii au tovuti yao.

“Kukosa kuzingatia yaliyo hapo juu kutahitaji timu kuendelea na hatua za kisheria na fidia,” barua hiyo ilieleza.

Katika video aliyopakia kwenye Snapchat na Insta Story yake, Zari alidai kuwa mpiga picha huyo alivujisha picha hizo kwa sababu alitaka kuwa wa kwanza kutangaza habari za likizo yake na mpenzi wake kwenye blogu yake.

Alilalamikia hatua hiyo na kusema kuwa mhusika alikosa weledi katika kazi yake na kukiuka makubaliano kati yake na hoteli. “Baadhi ya picha hizo ni nzuri na zingine kidogo ni PG 13,” alisema Zari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke