You are currently viewing ZARI THE BOSS LADY AMPA SOMO RAPPER WA KENYA JAPESA KWA KUTUMIA JINA LAKE VIBAYA

ZARI THE BOSS LADY AMPA SOMO RAPPER WA KENYA JAPESA KWA KUTUMIA JINA LAKE VIBAYA

Mrembo Zari The Bosslady amemshtumu Rapa wa Kenya Philip Okoyo almaarufu Japesa kwa kutumia jina lake kutafuta kiki huku akimuonya dhidi ya tabia hiyo.

Zari amesema kuwa madai ya hivi majuzi ya Rapa huyo kuwa wao ni marafiki wakubwa na huwa wanazungumza mara kwa mara ni ya uongo na hayana msingi wowote.

“Japesa sijawahi kuzungumza na wewe. Tafadhali toa wimbo wako kwa amani bila kutafuta kiki. Nachukia watu wanapotumia jina langu hivi,” amesema Zari.

Hivi majuzi, Japesa alitumia ukurasa wake wa Instagram kuchapisha screenshot ambazo alidai ni za mazungumzo yake na mama huyo wa watoto watano.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke